SERIKALI ya Jordan imewanyonga Wairaq wawili kwa kulipiza kisasi kwa kuuliwa raia mmoja wa nchi hiyo na kundi la Dola la Kiislamu.
Hatua hiyo ya kunyongwa imekuja saa chache baada ya kutolewa video inayoonesha rubani wa jeshi la Jordan akichomwa moto akiwa hai. Ripoti za televisheni ya taifa zinasema rubani huyo aliuwawa kiasi mwezi mmoja uliopita.
Mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati Randa Habib amesema mauaji hayo hayakubaliki kwa Muislamu wa kawaida.