CHUO KIKUU cha Makerere nchini Uganda kimeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kashfa ya shahada bandia katika chuo hicho.
Uchunguzi huo unataka kujua ni mazingira gani yaliyosababisha wanafunzi 600 kati ya wote waliofuzu zaidi ya elfu 11 kuwekwa katika orodha ya waliohitimu bila ya kufikisha viwango vya kuwafanya kufuzu.
Chuo kikuu cha Makerere kinaorodheshwa kama taasisi ya elimu ya saba bora katika kanda za Afrika mashariki na kati na Afrika Magharibi.