KAMPUNI ya Simu ya Push Mobile imetiliana saini na Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa -UN ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu Ugonjwa hatari wa Ebola.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Umoja wa Mataifa, Kampuni hiyo ya Simu imesema kupitia ushirikiano huo Kampuni hiyo itaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa Elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.
Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, Serikali na Wadau wake watatoa taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika.