WAZIRI wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema Urusi bado haijatimiza masharti ya makubaliano ya Minsk kuhusu usitishaji wa mapigano.
Kerry amewaambia wabunge mjini Washington kwamba Urusi na wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi hawaheshimu masharti ya makubaliano.
Wakati huo huo , rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba Urusi inaweza kusitisha upelekaji wa gesi nchini Ukraine. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameionya Urusi kwamba vikwazo vinaweza kutekelezwa.