Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Adam Johnson ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti mwenye umri wa miaka 15.
Polisi wa huko Durham wamethibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alifikishwa kwenye kituo hicho cha polisi kwa ajili ya mahojiano na baadae aliachiwa.
Kwa upande wa klabu ya Sunderland AFC mchezaji huyo kwa sasa amewekwa kando ili kupisha uchunguzi wa polisi, kukamatwa kwa mchezaji huyo wa ligi kuu ya Uingereza kuliripotiwa na gazeti la The sun