BUNGE LA MAREKANI LAIDHINISHA MABADILIKO MAPANA YA SHERIA YA UPELELEZI

BUNGE LA MAREKANI LAIDHINISHA MABADILIKO MAPANA YA SHERIA YA UPELELEZI

Like
225
0
Wednesday, 03 June 2015
Global News
BUNGE la Marekani limeidhinisha mabadiliko mapana katika sheria za upelelezi zilizopitishwa baada ya mashambulio ya kigaidi yaliyotokea Septemba 11mwaka wa 2001.
Mabadiliko hayo yaliuondoa mpango wenye utata wa Shirika la Usalama wa Kitaifa – NSA wa kukusanya data za mawasiliano ya simu unaowaathiri mamilioni ya Wamarekani kuchukuliwa sheria kali zaidi ya kuhifadhi rekodi hizo katika makampuni ya huduma za simu.
Sheria hiyo itafufua mipango mingi ambayo baraza la Seneti liliruhusu muda wake kumalizika ambapo tayari Rais wa Marekani Barack Obama ameuidhinisha muswada huo wa kihistoria wa Sheria ya Uhuru wa Marekani.

Comments are closed.