LIBERIA: KAMPUNI YA MAWESE YASHUTUMIWA KUJINUFAISHA KUPITIA MLIPUKO WA EBOLA

LIBERIA: KAMPUNI YA MAWESE YASHUTUMIWA KUJINUFAISHA KUPITIA MLIPUKO WA EBOLA

Like
258
0
Thursday, 23 July 2015
Global News

SHIRIKA moja la kutetea haki za binadamu limeishutumu mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mawese iliyoko nchini Liberia kwa kutumia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kujinufaisha.

Shirika hilo la Global Witness limesema kuwa wakati mlipukowa ugonjwa huo ulipoifikia Afrika Magharibi mwaka uliopita kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari kwa maandalizi ya kilimo cha zao la mawese wakati ambapo makundi ya misaada kwa jamii yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo.

Hata hivyo kampuni hiyo imejibu katika barua walioandika kwa shirika hilo la kuwa kandarasi ya pekee waliosaini mwaka huo ilitokana na kazi zao za miezi hadi miaka kadhaa kabla ya kuzuka kwa ugonjwa huo.

 

Comments are closed.