SERIKALI YAANZA KUTOA MAFUNZO KWA WATAALAM WATAKAOHUSIKA KUPITIA MIKATABA YA MADINI, GESI NA MAFUTA

SERIKALI YAANZA KUTOA MAFUNZO KWA WATAALAM WATAKAOHUSIKA KUPITIA MIKATABA YA MADINI, GESI NA MAFUTA

Like
192
0
Tuesday, 22 September 2015
Local News

ILI kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na rasilimali za madini mbalimbali pamoja na gesi iliyogunduliwa, Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka taasisi za serikali watakaohusika na upitiaji wa mikataba yote ya shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, gesi na mafuta kabla ya kusainiwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa George Simbachawene katika uzinduzi wa warsha kuhusu dira mpya ya madini Afrika iliyofanyika mjini Morogoro.
Warsha hiyo ya siku tatu iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini imewakutanisha wataalam kutoka taasisi za serikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais- Tume ya Mipango.

Comments are closed.