KUNDI linalopinga uhamiaji PEGIDA limehamasisha idadi kubwa ya watu wanaoliunga mkono katika mji wa mashariki nchini Ujerumani wa Dresden kujiunga na kundi hilo.
Kwa mujibu wa kundi huru la wanafunzi linalofanya utafiti la Durchgezält, mkutano wa PEGIDA ulihudhuriwa na watu kati ya Elfu kumi hadi Elfu kumi na mbili.
Lutz Bachmann, mmoja kati ya waasisi wa kundi hilo, alihutubia hadhara hiyo na kukosoa msimamo wa serikali ya kansela Angela Merkel, akidai imechukua uamuzi wa sera za uhamiaji bila ya kuwashauri wananchi.