RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli, asubuhi ya leo amemwapisha Bwana George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali –AG, herehe zilizo fanyika Ikulu jijini Dar es saalam.
Mwanasheria Mkuu Masaju ambaye kwa mara ya mwisho aliteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua nafasi hiyo iliyobaki wazi baada ya aliyekuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kujiuzulu.
Tayari Rais Dokta Magufuli ameshaitisha Vikao vya Bunge Novemba 17 na anatarajiwa kumtangaza Waziri Mkuu Novemba 19 mwaka huu.