106 WAPOTEZA MAISHA KWA KIPINDUPINDU TANGU AGOSTI 15

106 WAPOTEZA MAISHA KWA KIPINDUPINDU TANGU AGOSTI 15

Like
408
0
Tuesday, 10 November 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa tangu Agosti 15 Mwaka huu jumla ya Wagonjwa 106 wa kipindupindu wameshapoteza maaisha sawa na asilimia 1.3 ya idadi yote ya Wagonjwa 7825 walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Hellen Semu amesema jumla ya Wagonjwa 53 waliokuwepo katika Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wamepoteza maisha huku bado kukiwa na Wagonjwa katika vituo mbalimbali vinavyotumika kutibu wagonjwa wa kipindupindu.

 

Kwa upande wake Mratibu wa Kitengo cha Dharura  na Maafa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Mary Kitambi amesema kuwa ni lazima kila mtu kutambua kuwa ana jukumu la kulinda na kuzingatia usafi wa afya na mazingira ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa huo zaidi.

Comments are closed.