NCHI za Uganda na Kenya zimeimarisha usalama kufuatia mashambulio yaliyojitokeza mjini Paris mwishoni mwa wiki lengo ikiwa ni kuzuia mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu.
Msemaji wa polisi nchini Uganda amesema polisi na wanajeshi wameimarisha doria kuzuia mashambulio, hasa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab kutoka Somalia.
Nchini Kenya, usalama pia umeimarishwa mipakani na katika miji mikuu, na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka mara wanapoona kitu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka.