BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kikao chake cha kwanza kwa mchakato wa kumpata Spika wa Bunge hilo atakayeongoza kwa muda wa miaka mitano.
Miongoni mwa wagombea wanaowania Nafasi ya Uspika ni pamoja na Jobu Ndugai kutoka-CCM, Goodluck Ole Medeye wa CHADEMA, Peter Sarungi wa AFP, Hassan Almas kutoka NRA na Godfrey Malissa wa chama cha CCK.
Hata hivyo Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafuatiwa Zoezi la kuapishwa kwa wabunge wote.