WAZIRI wa Fedha na Mipango Dokta Philipo Mipango amesema kuwa wizara yake haitakuwa tayari kuona nchi ya Tanzania ikiendelea kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka nchi wahisani, bali itajiendesha kwa kukusanya mapato yakutosha yaliyopo ndani ya nchi ili jamii iweze kufaidika na matumizi ya mapato hayo.
Dokta mipango ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi ofisi aliyokuwa akikaimu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kabla ya kuapishwa kuwa waziri wa fedha na mipango kwa kamishna mkuu mpya wa mamlaka hiyo Alphayo Kidata ambaye awali alikuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi.