MANISPAA ya wilaya ya Ilala, imepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni kumi na mbili kutokana na kodi ya majengo kiasi kitakacho tumika katika kuboresha huduma za kijamii .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa uhusiano kutoka Manispaa hiyo, TABU SHAIBU amesema Manispaa ya Ilala ina vyanzo vingi vya mapato na moja ya vyanzo vikuu ni kodi ya majengo hivyo imepanga kuzunguka na kupita kila kona ya mtaa ili kuhakikisha ina wanakabiliana na wakwepa kodi ili kuongeza kuongeza mapato.