HATIMAYE, RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamefikia makubaliano ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kuhusiana na muundo wa serikali ya mpito.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali inaruhusiwa kuteua mawaziri 16, ambapo upande wa waasi wanaruhusiwa kuteua mawaziri 10.
Serikali ya mpito iliyokubaliwa itakuwa madarakani kwa miaka 3 kabla ya uchaguzi mpya kufanyika. Sudan Kusini imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuwawa.