WATU 70 wameuwawa wakati lori lililokuwa limewekewa miripuko kuripuka katika kambi ya polisi Kaskazini Magharibi ya Libya katika mji wa pwani wa Zliten.
Watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga, ambalo lilishambulia kundi la maafisa wa polisi waliokuwa wamekusanyika jana katika kambi .
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia, lori hilo lililokuwa na miripuko liligonga katika lango la kambi hiyo ambayo inatumiwa kuwapa mafunzo walinzi wa pwani.