SERIKALI imewataka wananchi kutunza barabara zinazojengwa na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika Halmashauri zote hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri nchini Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Mussa Iyombe
amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
Kwa mujibu wa Iyombe, Mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri za Iringa,Mufindi,Chamwino na Kondoa. Hata hivyo amewata wakurugenzi wa Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa kutunza barabara hizo ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.