SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kuwekeza zaidi katika ubora wa elimu na sio katika kutanua upatikanaji na nafasi ya elimu ili kutekeleza sera ya Elimu bure kwa Shule za Serikali kwa kuwa tafiti zinaonesha kuwa kiwango cha ufaulu katika miaka 10 iliyopita kimeshuka katika Shule za Msingi na Sekondari licha ya mfumo huo kutumika katika elimu ya msingi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti iliyotolewa na Twaweza kuhusu maoni ya Wananchi juu ya mabadiliko yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya elimu ya kuondoa michango yote ya Wazazi katika Shule za Serikali.