TANZANIA NA ZAMBIA ZIMETAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO

TANZANIA NA ZAMBIA ZIMETAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO

Like
182
0
Thursday, 25 February 2016
Local News

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Nchi Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kanda na Kimataifa Nchini,  imezitaka  Nchi za Tanzania na Zambia kuongeza ushirikiano ili kuleta mafanikio ya pamoja katika Sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na Biashara, Uchumi, Mawasiliano, Elimu, Utamaduni, Utalii,Kilimo pamoja na maswala ya Tekinolojia.

 

Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ramadhan Mwinyi alipozungumza  katika Ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Tume  ya  Kudumu ya Pamoja -JPC- kati ya Tanzania na Zambia ambapo amesema kupitia ushirikiano mwema kati ya Nchi hizo mbili zinaweza kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwenye Sekta hizo zilizokusudiwa na hatimaye kufikia malengo ya Tume hiyo.

Comments are closed.