IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaotumiwa na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuomba fedha barabarani wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutumia muda mwingi kwa kazi hiyo.
Akizungumza na EFM mwanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu, Jonathan Haule amesema kuwa watoto hao wamekuwa wakitembea barabarani nyakati za masomo.
Amesema kuwa ni vyema serikali ikaanzisha mifumo madhubuti itakayowawezesha watu wenye ulemavu kufanya kazi zao pasipo kutegemea msaidizi.