WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Like
242
0
Tuesday, 03 May 2016
Local News

MAMLAKA ya hali ya hewa Nchini-TMA-imewataka Wakulima na Wafugaji kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji katika kilimo na Ufugaji.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya hali ya hewa Nchini Dokta Ladislaus Chang’a amesema  mifugo mingi pamoja na mazao ya kilimo yamekuwa yakiharibika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa jambo ambalo  husababisha upungufu katika uzalishaji hivyo ni muhimu kwa wakulima hao kufuatilia taarifa hizo.

Dokta Chang’a amewataka Wakulima na Wafugaji kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka na kuacha ukataji miti ovyo ili kudhibiti athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Comments are closed.