WABUNGE WA UPINZANI WATINGA NA MABOMU YA MACHOZI BUNGENI
Wabunge wa upinzani nchini Kosovo wamerusha mabomu ya machozi katika ukumbi wa bunge nchini humo wakiwa na lengo la kukwamisha mpango wa kupiga kura za maoni juu ya makubaliano ya mpangilio wa mpaka kati ya Kosovo na Montenegro.
Mpango huo uliotakiwa kuanza jumatano ya leo ulikwama baada ya
Wabunge hao wa Chama cha Self-Determination Movement kulazimisha wabunge kutawanyika na kutoka nje ya Bunge.
Jumla ya kura 120 zilitarajiwa kukusanywa bungeni hapo ambapo theluthi mbili zinahitajika kuthibitisha mkataba wa 2015 .