Kenya Yapiga Marufuku Kuwatembelea Watoto Shuleni

Kenya Yapiga Marufuku Kuwatembelea Watoto Shuleni

Like
642
0
Wednesday, 06 June 2018
Global News

Wizara ya Elimu nchini Kenya imeivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls na kutangaza kwamba ni marufuku kuwatembelea watoto shuleni baada ya mapumziko ya katikati ya muhula kwa shule zote za upili za umma.

Hii ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kubaini kesi ya ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo.

Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed alitoa agizo kwa maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote kuepuka uwezekano wa wanafunzi kuingiliwa.

Mwalimu mkuu katika shule ya upili ya Moi Girls amewasilisha ombi kwa tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, kutaka kustaafu mapema baada ya kuzuka tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo mwishoni mwa juma ndani ya shule hiyo.

Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wakiume katika shule ya upili ya Moi Girls Nairobi wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa DNA wakati maafisa wa upelelezi wanajaribu kuchunguza tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa usiku.

Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa kiume wa walimu wanaoishi ndani ya Shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi.

Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumithilisha mshukiwa dhidi ya maji maji yanayopatikana katika mwili wa muathiriwa na hivyo kuweza kuwana ushahidi mzito katika kesi.

Itasaidia pia kubaini iwapo washukiwa wataokaochunguzwa walikuwa katika eneo la tukio hilo la uhalifu au kuwaondoshea makosa yoyote.

Polisi wanajaribu kuchunguza matukio yaliojiri usiku huo wa mkasa na siku ya pili iliyofuata kujua ukweli upo wapi katika tuhuma hizo za kubakwa kwa wanafunzi wa Moi Girls ambazo zimezusha hasira kubwa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *