Chama cha Trump, Republicans chabanwa mbavu katika uchaguzi

Chama cha Trump, Republicans chabanwa mbavu katika uchaguzi

Like
492
0
Wednesday, 07 November 2018
Global News

Chama cha Rais Donald Trump, Republicans kinaelekea kupoteza wingi katika bunge la Congress hali ambayo iatafanya urais wa Trump kupitia katika wakati mgumu zaidi.

Hata hivyo, chama cha Republicans kinatarajiwa kuendelea kuwa na wingi katika Magavana na viti vya bunge la Seneti.

Kwenye uchaguzi wa bunge la Congress, mpaka sasa majimbo 383 yametangaza matokeo. Democrats wanaongoza kwa viti 200 huku Republicans wakifuatia na viti 183. Bado kuna majimbo ya uchaguzi 52 hayajatangaza matokeo na Democrats wanatarajia kushinda zaidi. Katika uchaguzi kama huu mwaka 2014 Republicans walizoa viti 247 na huku Democrats wakiambulia viti 188.

Ushindi wa Democrats katika bunge la Congress, si jambo zuri hata kidogo kwa Rais Trump ambapo sasa atakabiliwa na upinzania maradufu katika kutekeleza sera zake kwa miaka miwili iliyobaki kwenye muhula wake wa uongozi.

Upande wa bunge la Seneti mpaka sasa kati ya majimbo 94 yaliyotangaza matokeo, Republican wameshinda 51 na Democrats 42. Bado majimbo manne hayatangaza matokeo. Katika uchaguzi kama huu uliofanyika mwaka 2014, Republicans walishinda viti 54 huku Democrats wakipata viti 46.

Katika upande wa Magavana, tayari majimbo 45 yameshatangaza matokeo huku Republican wakiongoza kwa kuwa na viti 25 na Democrats 20. Bado kuna majimbo matano hayajatangaza matokeo. Mwaka 2014 Republicans walishinda majimbo 37 na Democrats 17.

NEW YORK, USA – SEPTEMBER 21: US President Donald Trump is seen during his meeting with Turkish President Recep Tayyip Erdogan (not seen), at Lotte Hotel in New York, United States on September 21, 2017. World leaders gathered in New York for the 72nd Session of the UN General Assembly.
(Photo by Volkan Furuncu/Anadolu Agency/Getty Images)

Uchaguzi huu wa katikati ya muhula unakuja wakati rais Trump amefikia nusu ya muda wa uongozi wake madarakani.

Uchaguzi huu pia unatarajiwa kubaini ikiwa Trump ana uwezo wa kuongoza Marekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Shauku ya upigaji kura hususani kwa vijana ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2014.

Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake.

Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama – amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za chama cha Democratic – amesema “hulka ya taifaletu iko katika sanduku la upigaji kura”.

Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake.

Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama – amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za chama cha Democratic – amesema “hulka ya taifaletu iko katika sanduku la upigaji kura”.

Wagombea wa Democratic kwa upande wao wameamua kujiepusha na makabiliano ya moja kwa moja na wapinzani wao na badala yake kuangazia masuala ibuka kama vile ya afya na ukosefu wa usawa katika mambo ya uchumi.

Chama hicho kinatumai kuwa wapiga kura vijana na wale wanaotokea katika makundi ya wachache waliyotengwa watavutiwa na kura hiyo kama hatua ya kupinga msimamo wa rais Trump dhidi ya masuala yanayowagusa wao na wenzao moja kwa moja.

Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na lugha yake ambayo inadaiwa kuwagawanya watu.

Watafiti wa kura ya maoni wanabashiri kuwa Democrats huenda wakashinda viti 23 wanavyohitaji kuongoza bunge la waalikilishi , na viti vingine zaidi kama 15 za ziada.

Uchaguzi huu unamaanisha nini?

Uchaguzi wa katikati ya muhula utaamua ni nani atakayechukua udhibiti wa mabunge yote mawili ambayo yanatunga sheria ya nchi.

Ikiwa Republicans watafanikiwa kuendelea kuongoza mabunge ya seneti na ya uwakilishi, huenda wakaimarisha ajenda ya chama na ile ya rais Trump.

Lakini Democrats wakiwapokonya jukumu hilo huenda wakabadilisha mipango ya bwana Trump.

Katika mahojiano na runinga ya ABC siku ya Jumatatu, rais Trump alisema anataka kupunguza makali ya matamshi yake katika kipindi kilichosalia cha uongozi wake.

“Nahisi kwa kiwango fulani, sina chaguo, nadhani nilitakiwa kupunguza makali ya matamshi yangu kuanzia mwanzo.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *