Morocco imezindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika – itakayopunguza nusu ya muda unaotumika kusafiri katika miji ya kibiashara na kiviwanda Casablanca na Tangi
Mfalme Mohammed VI na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliipanda treni hiyo katika safari ya uzinduzi kutoka Tangier hadi katika mji mkuu Rabat.
Afrika inatazamia kuimarisha miundo mbinu ya usafiri kushinikiza biashara, uwiano na utangamano wa kieneo.
Mataifa ya Afrika yanakumbatia mfumo wa reli ya mwendo kasi katika kujaribu kushinikiza na kukuza uchumi na kuimarisha kasi za kusafirisha bidhaa baina ya mataifa kibiashara.
Katika miaka 20 iliyopita jitihada za kufufu mfumo wa reli umechangi baadhiya maatifa kuamua kubinafsisha huduma hizo hususan katika mataifa ya magharibi na mashariki ya Afrika.