Mourinho agoma kuzungumzia kufutwa kazi

Mourinho agoma kuzungumzia kufutwa kazi

Like
623
0
Thursday, 20 December 2018
Sports

Jose Mourinho anasema kwamba, hawezi kuzungumzia kuhusu kuondoka kwake kutoka kwenye ukufunzi mkuu wa timu ya soka ya Manchester United, kwa sababu ya “heshima kubwa aliyo nayo” kwa Mashetani Wekundu.

Mreno huyo alifutwa kazi siku ya Jumanne baada ya kukifunza timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili u nusu.

Timu ya Man United ipo kwenye nafasi ya 6 katika jedwali la mchuano wa Ligi kuu ya Premia, alama 19 nyuma ya viongozi Liverpool.

“Nilikuwa na furaha kubwa kuvalia nembo ya Manchester United, tangu siku ya kwanza kufika hapa, na nina imani kuwa mashabiki wote wa Man United, walitambua hilo,” Mourinho amesema kwa njia ya taarifa.

“Kila mara ukurasa unapofungwa, mimi huonyesha heshima kubwa kwa kutosema lolote kuwahusu wenzangu wa zamani.”

Siku ya Jumatano, mshambulizi wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, aliteuliwa kusimamia kwa muda klabu hiyo, hadi mwisho wa msimu huu.

Mourinho amekwenda nyumbani kwake Jijini London, huku mkufunzi huyo wa zamani wa timu za Chelsea na Real Madrid, akiviomba vyombo vya habari kumpa heshima na kutoingilia mambo yake ya ndani, kabla hajarejea tena katika ukufunzi wa soka.

kizungumza na Sky Sports News, mapema siku ya Jumatano, alisema: “Daima nilikuwa nashangazwa sana na wakufunzi wanaohama hama vilabu vya soka, na kisha wanaanza kuzungumzia maswala ya ndani ya kile kilichotokea, hasa ni nani wa kulaumiwa.

“Siwezi kabisa kuzungumzia kitu ambacho hakikuwa kizuri, huyo sio mimi kabisa.

“Hadi nitakaporejea tena kwenye ulingo wa soka, kwa sasa napenda kuishi maisha yangu tu ya kawaida. “Hatma ya baadaye ya Manchester United iko nzuri bila ya mimi, na pia mimi maisha yangu ya baadaye ni nzuri mno bila ya Manchester United.”…Hiyo ndio taarifa ya kina ya Mourinho.

Salamu kamili za Mourinho

Nimekuwa na furaha isiyo na kifani kuvalia nembo ya Manchester United, tangu siku ya kwanza nilipowasili Old Traford, na nina amini kuwa mashabiki wote wa Man U wanatambua hilo.

Na hivyo ndivyo ilivyo tu na vilabu vyangu vya awali, ambako nilifanya kazi, nimefanya kazi na watu wazuri na nina imani kuwa baadhi yao watakuwa marafiki zangu milele.

Najua kuwa mnafahamu misingi yangu ya kazi na taaluma yangu. Kila mara ukurasa unapofungwa, mimi huonyesha heshima ya dhati mno kwa wenzangu wa zamani.

Nadhani vyombo vya habari vitaheshimu msimamo wangu na kuniacha niishi tu maisha ya kawaida, hadi pale nitakapoamua kurejea tena katika ukufunzi wa soka.

Krismasi njema

Maoni ya wachezaji

Mchezaji wa kiungo cha kati Jesse Lingard, alikuwa mchezaji wa kwanza kabisa kumuandikia Mourinho ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, “Thank you for the memories and wisdom,” yaani “Asante kwa kumbukumbu na busara yako.”

Naye mlinzi wa kati Eric Bailly aliandika: “Lolote wasemalo, daima nitamshukuru mtu aliyenipa fursa ya kubobea katika uwanja wa Old Trafford.

“Asante sana kwa kile ulichonifunza. Heri njema Kocha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *