Utepe mweupe watoa ujumbe kwa jamii

Utepe mweupe watoa ujumbe kwa jamii

Like
731
0
Monday, 18 March 2019
Local News

Wadau wa sekta ya Afya wameazimisha siku ya Muungano wa Utepe mweupe wa uzazi salama katika mkoa wa Kagera kwa kuhimiza jamii kuzuia ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana

Maazimisho hayo yamefanyika katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera yakiwa na kauli mbiu ‘komesha  unyanyasaji kwa wanawake na wasichana, okoa maisha wakati wa uzazi’.

Meneja Mawasiliano wa Muungano wa Utepe mweupe wa uzazi salama, Anna sawaki amesema kuwa lengo la kufanya maazimisho ni kuweza kupunguza vifo kwa wanawake wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa takwimu zinaonyesha vifo vitokanavyo na uzazi vinaongezeka badala ya kupungua kutokana na unyanyasaji wanaoupata akina mama pindi wawapo wajawazito na wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake mratibu wa taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama, Rose Mlayi ameiomba jamii  kukomesha ukatili kwa wanawake na wasichana, ili kuokoa maisha yao wakati wa uzazi.

Katika hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo amesisitiza kuwa serikali kupitia idara zake inaendelea kukomesha vitendo hivyo, ikiwemo kuendelea na mikakati yake ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi.

Waziri ummy ameongeza kuwa wizara yake inaendelea kuboresha sekta ya afya hasa upande wa vituo vya afya pamoja na vifaa tiba ambapo pia ameeleza mkakati wa kuanzisha vituo vya huduma jumuishi kwa kila kituo cha afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *