‘Licha ya juhudi zao marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo”

‘Licha ya juhudi zao marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo”

Like
686
0
Thursday, 04 April 2019
Global News

Ripoti ya uchunguzi kuhusu kuanguka kwa ndege ya Ethiopia Airlines mwezi uliopita inasema kuwa ndege hiyo ilitaka kuangukia pua yake mara kadhaa kabla ya ajali hiyo.

Marubani walifuata maagizo yaliopendekezwa na Boeing kabla ya ajali hiyo kulingana na ripoti ya kwanza ya ajali hiyo.

”Licha ya juhudi zao , marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo” , alisema waziri wa uchukuzi Dagmawit Moges.

Ndege hiyo aina ya ET302 ilianguka baada ya kupaa kutoka mji wa Adis Ababa , na hivyobasi kuwaua watu 157.

Ilikuwa ndege ya pili aina ya Boeing 737 kuanguka katika kipindi cha miezi mitano.

Mwezi Oktoba mwaka uliopita , ndege aina ya Lion Airflight JT610 ilianguka baharini karibu na Indonesia na kuwaua watu wote waliokuwa wameabiri.

”Wafanyikazi wa ndege hiyo walijaribu kila mbinu walizoelezewa na mtengenezaji wa ndege hiyo lakini walishindwa kuidhibiti” , bi Moges alisema katika mkutano na wanahabari mjini Adis Ababa.

Katika taarifa , afisa mkuu wa Ethiopia Airlines , Tewolde GebreMariam alisema kuwa alifurahishwa na kazi ya marubani hao kujaribu kuidhibiti ndege hiyo.

”Ni bahati mbaya kwamba walishindwa kuidhibiti ndege hiyo kutoangukia pua yake”, ilisema kampuni hiyo ya ndege katika taarifa yake.

Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines CEO Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na :

Wakenya 32 Kenyans, raia wa Canada 18 raia tisa wa Ethiopia , wataliano wanane , Wachina wanane, wamarekani wanane , waingereza saba , Wafaransa saba , Wamisri sita, Wajerumani watano , Wahindi wanne na wanne kutoka Slovakia.

Waaustralia watatu, Waswizi watatu, Warusi watatu , Warusi 3, Wakomoro wawili, Wahispania wawili, Wapoland wawili, Waisraeli wawili.

Kulikuwa pia na abiria mmoja kutoka nchi za Ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, Togo, Msumbiji, Rwanda, Sudan, Uganda na Yemen.

Boeing ambayo ni kampuni ambayo iliitengeneza ndege iliyoanguka , imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba ‘inafuatilia kwa karibu hali’ ya mambo.

Ndege ya 737 Max-8 ni mpya angani , ikiwa ilizinduliwa kwa mara ya kwanza 2016. Iliongezwa kwenye safari za ndege za Ethiopian Airlines Julai mwaka jana.

Boeing imesema ”imesikitishwa sana” na ajali na imejitolea kutuma kikosi cha wahandisi wake kutoa usaidizi wa kiufundi.

Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *