ADAM JOHNSON AKABILIWA NA KESI YA KUWA MAHUSIANO NA MTOTO WA MIAKA 15

ADAM JOHNSON AKABILIWA NA KESI YA KUWA MAHUSIANO NA MTOTO WA MIAKA 15

Like
334
0
Wednesday, 04 March 2015
Slider

Mshambuliaji wa klabu ya  Sunderland  Adam Johnson ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti mwenye umri wa miaka 15.

Polisi wa huko Durham wamethibitisha kuwa  mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alifikishwa kwenye kituo hicho cha polisi kwa ajili ya mahojiano na baadae aliachiwa.

Kwa upande wa klabu ya Sunderland AFC mchezaji huyo kwa sasa amewekwa kando ili kupisha uchunguzi wa polisi, kukamatwa kwa mchezaji huyo wa ligi kuu ya Uingereza kuliripotiwa na gazeti la The sun

Comments are closed.