AFCON: BAADA YA MBABE KUKOSEKANA KUNDI B LEO TIMU ZA KUNDI C ZITASHUKA DIMBANI

AFCON: BAADA YA MBABE KUKOSEKANA KUNDI B LEO TIMU ZA KUNDI C ZITASHUKA DIMBANI

Like
319
0
Monday, 19 January 2015
Slider

Mataifa yanayounda kundi B ambayo ni Drc, Tunisia, Cape verde na Zambia katika michuano ya kombe la mtaifa Afrika zimejikuta zikikosa mbabe baada timu zote kuibuka na sare ya kufungana 1-1

 Mchezo wa kwanza wa kundi hilo ulipigwa kwakuikutanisha Zambia na Congo ambapo Zambia ilitangulia kuziona nyavu za Drc kupitia mnamo dakika ya pili bao lililofungwa na mchezaji wake Given Singuluma na kudumu hadi mapumziko

Bao hilo lilisawazishwa na mchezaji wa Drc Yannick Bolasie kwenye dakika ya 66 hadi mwisho wa mchezo ambapo timu zote ziliibuka na pointi moja

 

Cape verde ilishuka dimbani na Tunisia katika mchezo wa pili wa kundi B ambapo Tunisia ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 70 lililofungwa na Ali Moncer ambapo dakika 7 baadae Cape verde ilisawazisha bao hilo kupitia mchezaji wake Almeida Ramos, mchezo huo pia ulimalizika kwa sare ya kufungana1-1

Leo ni mechi za kundi C ambapo Ghana itaonyeshana kazi na Senegal, zikifuatiwa na mchezo kati ya Algeria na Afrika Kusini.

Kundi A linaongozwa na timu ya Gabon ambayo iliirarua Burkina Faso 2-0 katika mchezo wa Jumamosi, huku wenyeji Equatorial Guinea wakitoka sare ya 1-1 na Congo.

Comments are closed.