AFCON: MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA AFRIKA KUSINI

AFCON: MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA AFRIKA KUSINI

Like
270
0
Tuesday, 20 January 2015
Slider

Ikiwa michuano ya Afcon tayari imeanza kwenye hatua za makundi huko EQUTORIAL GUINEA   macho yetu leo hii yanalitazama taifa la Afrika kusini, Afrika kusini ni nchi inayopatikana kusini mwa bara la Afrika ikiwa karibu na bahari ya Atlantic na bahari ya Hindi,nchi hiyo imepakana na Zimbabwe,Botswana,Namibia,Lesotho na Swaziland.Taifa hilo limepata uhuru kutoka kwa wadachi mwaka 1994

Afrika kusini ni nchi ya pili inayoongoza kiuchumi barani Afrika na inashika nafasi ya 34 kiuchumi duniani, Taifa la Afrika Kusini linamchanganyiko wa watu wa aina mbalimbali duniani na Taifa hilo linatumia jumla ya lugha 11 ambazo zote ni rasmi.Maendeleo ya Taifa hilo yanakuja kutokana na kuendelea katika teknolojia,kiviwanda,miundombinu na uongozi bora.

Afrika kusini ina makabila zaidi ya 10 na kabila kubwa nchini humo ni wazulu, taifa hilo lina raia milioni 54 na 2000.

Katika soka Timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana imeshiriki mara 8 katika michuano hiyo ya AFCON ikichukua kombe hilo mara moja mwaka 1996 walipokua wenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Taifa hilo linaenda katika michuano hiyo likiwa na pigo la kumpoteza nahodha wao SENZO MEYIWA aliyefariki 26 October 2014 baada ya kupigwa risasi mbele ya mpenzi wake KELLY KHUMALO

Katika michuano ya AFCON mwaka huu Bafana Bafana ipo katika kundi C pamoja na Ghana,Senegal na Algeria,mchezo wa kwanza Bafana Bafana ulichezwa jana wakati timu hiyo iliposhuka dimbani kuminyana na Algeria siku ya tarehe 19/mwezi huu saa 3 usiku katika uwanja wa estadio de mongomo uliopo mjini mongomo na matokeo ya mchezo huo Algeria iliibuka na ushindi wa mabao 3-1

 

 

Comments are closed.