AFRIKA KUSINI: POLISI WANANE WAFUNGWA JELA

AFRIKA KUSINI: POLISI WANANE WAFUNGWA JELA

Like
221
0
Wednesday, 11 November 2015
Global News

MAAFISA wanane wa polisi waliopatikana na hatia ya kumfanyia ukatili dereva wa teksi kutoka Msumbiji mwaka 2013 wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja.

Maafisa hao walinaswa kwenye kanda ya video wakimburuza dereva wa gari ndogo (teksi) kutoka Msumbuji aliyetambuliwa kwa jina la Macia mwenye umri wa miaka 27 mtaa wa Macia mashariki mwa Johannesburg.

Awali kabla ya kutokea kwa tukio hilo Macia alikuwa amesimamishwa na maafisa tisa wa polisi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama barabarani.

Comments are closed.