AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI ITAKAYOGHARIMU SHILINGI MILIONI MIA TISA

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI ITAKAYOGHARIMU SHILINGI MILIONI MIA TISA

Like
602
0
Monday, 02 February 2015
Local News

KAMPUNI ya simu za Airtel, leo imezindua promosheni kabambe itakayogharimu shilingi milioni mia tisa ijulikanayo kama airtel yatosha zaidi ,itakayomuwezesha mteja wake kijishindia gari aina ya Toyota IST.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa masoko ya airtel, Levi Nyakundi amesema promosheni hiyo ni nafasi ya pekee kwa wateja wao wanaojiunga na vifurushi vya airtel yatosha zaidi vya siku,wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana na pesa wanazozitumia, lengo likiwa ni kuhakikisha wanatoa huduma na bidhaa bora kwao.

Nyankundi amesema ni imani yao kuwa promosheni hiyo itawapatia wateja wao uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma za airtel yatosha zaidi, kwani wateja 60 watajishindia gari aina ya Toyota IST kila siku yenye thamani ya milioni 15 kila moja kwa muda wa miezi miwili.

Naye Mkurugenzi wa mawasiliano wa airtel Beatrice Singano Mallya amesema ili kushiriki kwenye promosheni hiyo wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya yatosha vya siku ,wiki na mwezi na hakuna gharama ya zaidi

IMG_5358 IMG_5375 IMG_5377 IMG_5380 IMG_5383 IMG_5401 IMG_5407

Comments are closed.