JESHI LA NIGERIA LAFANIKIWA KUSAMBARATISHA SHAMBULIO LA PILI LA BOKO HARAM

JESHI LA NIGERIA LAFANIKIWA KUSAMBARATISHA SHAMBULIO LA PILI LA BOKO HARAM

Like
200
0
Monday, 02 February 2015
Global News

JESHI la Nigeria limesema kuwa limefaulu kusambaratisha shambulio la pili la Boko Haram, juma moja tu baada ya kusambaratisha jaribio jingine la mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Maiduguri.

Msemaji wa jeshi hilo Meja Jenerali Chris Olukade, amesema kuwa waliwauwa waasi wengi wa Boko Haram katika shambulio hilo lililotokea mapema Alfajiri leo, huku wakipata bunduki, risasi na magari yaliyokuwa yakitumika na waasi hao wa Boko Haram.

Lakini wapiganaji wa vijijini wameliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa wanakanusha hilo na kusema wanajeshi waliogopa na kutoroka na hakuna dalili zozote za ndege za kijeshi katika eneo hilo.

Comments are closed.