AJALI YA BASI LA SIMIYU EXPRESS YAUA WATU 10

AJALI YA BASI LA SIMIYU EXPRESS YAUA WATU 10

Like
730
0
Thursday, 23 July 2015
Local News

WATU kumi wamefariki dunia papo hapo na wengine 47 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya simiyu express lililokuwa likitokea bariadi mkoani simiyu kuelekea jijini dar es salaam kupasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo na kisha kuparamia mti katika kijiji cha Wilunze eneo la Chalinze nyama wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kabla ya ajali, basi hilo lenye namba za usajili T 318 ABM Scania lilikuwa kwenye mwendo mkali na wakasikia kishindo cha kupasuka kwa tairi.

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kamishina masaidizi David Mnyambugha amesema ni mwendo kasi ambapo mara baada ya tairi kupasuka   na Dereva kushindwa  kulimiliki na ndipo likapoteza mwelekeo

Comments are closed.