AMNESTY INTERNATIONAL: NCHI ZA ULAYA ZINAKIUKA HAKI ZA BINADAM MIPAKANI

AMNESTY INTERNATIONAL: NCHI ZA ULAYA ZINAKIUKA HAKI ZA BINADAM MIPAKANI

Like
246
0
Wednesday, 18 November 2015
Global News

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, limesema uzio wa mipakani na udhibiti mwingine unaofanywa na mataifa ya Umoja wa Ulaya vinachochea ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Mkurugenzi wa shirika hilo barani Ulaya na Asia ya Kati John Dalhuisen, amesema kutanua uzio katika mipaka ya Ulaya kumechochea changamoto za kudhibiti wimbi la wakimbizi kwa njia za kistaarabu, na utaratibu mzuri.

Ripoti hiyo imeangalia athari zinazosababishwa na uzio mpya, hasa katika mpaka wa Hungary na Serbia na wajibu wa mataifa kama Uturuki na Morocco katika utetezi wa haki za binadamu.

Comments are closed.