AMNESTY YAKOSOA SERIKALI ULIMWENGUNI KUSHINDWA KUWALINDA RAIA

AMNESTY YAKOSOA SERIKALI ULIMWENGUNI KUSHINDWA KUWALINDA RAIA

Like
167
0
Wednesday, 25 February 2015
Global News

SHIRIKA la haki za binaadamu la Amnesty International limezikosoa serikali ulimwenguni kwa kushindwa kuwalinda mamilioni ya raia dhidi mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola na makundi yenye silaha.

Ripoti ya kila mwaka iliyochapishwa leo na shirika hilo inaelezea hatua ambazo zimechukuliwa na ulimwengu dhidi ya migogoro nchini Nigeria na Syria kuwa ni za kutia aibu.

Amnesty International inayalaumu mataifa tajiri duniani kwa kutumia nguvu na fedha nyingi kuwazuia watu kuingia kwenye mataifa hayo, kuliko kuwasaidia watu kuishi.

 

Comments are closed.