KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL ameeleza kuunga kwake mkono mpango mpya wa uwekezaji katika Bara la Ulaya.
Mpango huo wa Uwekezaji umependekezwa mwaka jana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya JEAN-CLAUDE JUNCKER ambapo ni mpango wa Euro Bilioni 300 wa kuifanya bora miundo Mbinu katika mataifa ya Ulaya.
MERKEL ameeleza uungaji wake mkono katika mpango huo , lakini amesema mageuzi zaidi na makubaliano ya Biashara huru na Marekani na Canada yanahitajika.