HOSPITALI ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Figo-NESOT pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya na Magonjwa ya Figo, imeeleza kuwa Ugonjwa wa Figo wa Mstuko na Ugonjwa Sugu wa Figo ni tatizo mojawapo kwenye kundi la magonjwa yasiyoambukiza ambayo mchango wake katika kuongeza athari za Kiafya na Vifo Ulimwenguni unaongezeka siku hadi siku.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo, Dokta JACKLINE SHOO amesema Tanzania ni nchi ya 54 katika nchi zinazoongoza kwa vifo ambapo asilimia 1.03 ya Watanzania hufariki kila mwakakwa ugonjwa wa Figo