BAADA YA YANGA JANA KUCHEZEA KICHAPO CHA 3-1 LEO NI ZAMU YA SIMBA

BAADA YA YANGA JANA KUCHEZEA KICHAPO CHA 3-1 LEO NI ZAMU YA SIMBA

Like
962
0
Monday, 04 June 2018
Sports

Baada ya Yanga Sc kutupwa nje kwenye mashindano ya Super cup nchini Kenya kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Kakamega Homeboys, leo ni zamu ya Simba SC kutupa karata yake ya kwanza katika michuano ya hiyo ya Super Cup inayoendelea Nakuru nchini Kenya watacheza na .Kariobang Sharks majira ya saa tisa alasiri

Kuelekea mechi hiyo, Simba wamedhamiria kupigania matokeo chanya huku wakiahidi kutokufanya vibaya kama ilivyokuwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, amesema wameamua kuiwekea msisitizo awamu hii michuano hiyo ili kupata nafasi ya kucheza na Everton huko Goodison Park, England, na hii ni endapo watakuwa mabingwa.

Kufanya vizuri kwa Simba leo kutakuwa kunawafariji watani zake wa jadi Yanga waliotolewa jana na KK HomeBoys pamoja na JKU iliyoondoshwa na Gor Mahia FC.

Ikumbukwe katika mashindano hayo yaliyfanyika Dar es Salaam mwaka jana, Simba na Yanga walitumia wachezaji wa kikosi cha pili na badala yake wakashindwa kukitwaa kikombe kilichochukuliwa na Gor Mahia FC.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *