SERIKALI ya Tanzania imesema imeshtushwa na Ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China
Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa Kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo.
Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya Rais wao nchini kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za ndovu.