KIASI cha watu 15 wameuawa kufuatia shambulizi la kujitoa muhanga linalodaiwa kufanywa na watu wawili wanaoshukiwa kuwa na mahusiano na wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu katika eneo la msikiti wa kishia mjini Baghdad.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya madaktari na polisi watu wengine 50 wanadaiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.
Duru zinaarifu kuwa mtu wa kwanza alijitoa muhanga na kufuatiwa na wa pili ambaye pia alijilipua baada ya maafisa usalama kufika katika eneo hilo na kuongeza kuwa baadhi ya wahanga wa tukio hilo ni maafisa wa vyombo vya usalama nchini humo.