BAN KIN MOON AZITAKA NCHI ZENYE NGUVU KUTIMIZA AHADI ZAO

BAN KIN MOON AZITAKA NCHI ZENYE NGUVU KUTIMIZA AHADI ZAO

Like
217
0
Friday, 04 December 2015
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani lazima zitimize ahadi zao za kuchangisha kiasi cha dola bilioni 100 kufadhili juhudi za kulinda mazingira ifikapo mwaka 2020.

Ban Ki-moon amewaambia wanahabari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa nchi zinazostawi zinataka msimamo thabiti kuhusu ufadhili huo uliokubalika katika mkutano wa kilele wa mazingira mjini Copenhagen, Denmark mwaka 2009.

Nchi maskini zinatafuta mabilioni ya fedha ili kuepusha athari za kutolewa kwa gesi chafu inayoongeza kiwango cha joto duniani. Mkutano huo wa kilele wa mazingira unaoendelea Paris, Ufaransa.

Comments are closed.