BOKO HARAM YADAIWA KUENEA LAGOS

BOKO HARAM YADAIWA KUENEA LAGOS

Like
206
0
Monday, 31 August 2015
Global News

MAAFISA wa Serikali nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, wanajaribu kupanua shughuli zao kutoka maeneo ya Kaskazini, yenye idadi kubwa ya Waislamu, hadi mji mkuu wa Lagos na maeneo mengine.

Wakati huo huo idara ya ujasusi nchini humo imesema kuwa imewakamata takriban makamanda 20 wa kundi hilo la Boko Haram.

Aidha idara hiyo imesema kuwa wapiganaji wengine wamekamatwa katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa nchi hiyo yakiwemo ya Kano, Gombe , Central Plateau, pamoja na maeneo ya Lagos Kusini na Enugu kati ya Julai na Agosti mwaka huu.

 

Comments are closed.