BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA

BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA

Like
201
0
Friday, 03 July 2015
Global News

IMEELEZWA kwamba jumla ya Watu 150 wameuawa baada ya kundi la Boko Haram kuvamia na kufanya mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi ya  Nigeria.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa mashambulizi hayo zinasema kuwa watu tisini na saba wameuawa katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad kutokana na mashambulizi hayo.

Hata hivyo baadhi ya Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wamesema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wamewaua wanaume, wanawake na watoto.

Comments are closed.