BUNGE LAPITISHA MUSWADA KUZUIA VITENDO VYA UHARAMIA DHIDI YA MIUNDOMBINU

BUNGE LAPITISHA MUSWADA KUZUIA VITENDO VYA UHARAMIA DHIDI YA MIUNDOMBINU

Like
228
0
Monday, 24 November 2014
Local News

BUNGE LA JAMHURI ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Azimio la Bunge kuridhia Itifaki ya kuzuia vitendo vya uharamia dhidi ya Miundombinu ya Kudumu iliyojengwa chini ya Bahari ya mwambao wa Bara ya mwaka 1988 iliyowasilishwa November 21 mwaka huu na Waziri wa Uchukuzi Dokta HARRISON MWAKYEMBE.

Muswada huo umepitishwa leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya Wabunge kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo ya maboresho ambayo yatawezesha kukomesha vitendo vya uharamia katika masuala mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine suala la -ESCROW limeendelea kuibua hisia tofauti kwa baadhi ya Wabunge kufuatia Mwongozo ulioombwa na Mheshimiwa JAMES MBATIA juu ya taarifa ya kusambaa kwa ripoti ya –CAG katika maeneo mbalimbali ambapo ufafanuzi wa suala hilo umetolewa na Spika wa Bunge Mheshimiwa ANNE MAKINDA.

 

Comments are closed.