BURUNDI: KIONGOZI WA UPINZANI AHUDHURIA KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE

BURUNDI: KIONGOZI WA UPINZANI AHUDHURIA KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE

Like
198
0
Tuesday, 28 July 2015
Global News

KIONGOZI wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa amehudhuria kikao cha kwanza cha bunge tangu kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge june 29 mwaka huu.

Hatua hiyo imewashangaza watu wengi kwa kuwa awali alipinga matokeo ya uchaguzi huo pamoja na yale ya urais wiki iliopita ambapo alijipatia asilimia 20 ya kura katika uchaguzi mkuu.

Hata hivyo viti 12 kati ya 30 vya muungano wake havikuwa na wabunge huku wabunge walio watiifu kwa kiongozi mwenza Charles Nditije wakisusia kikao hicho.

Comments are closed.