Local News

TWENDE SAWA: EFM KUADHIMISHA MWAKA MMOJA
Local News

KATIKA kusheherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kituo hiki cha Efm – 93.7, tarehe 2/4/2014 , imeelezwa kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wasikilizaji wa Radio hii ambayo imejipatia umaarufu mkubwa Katika kipindi cha muda mfupi, ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wasikilizaji wake. Akizungumza na wandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Mawasiliano wa Efm, Denis Ssebo, amesema Sherehe hizo ambazo zimepewa kauli mbiu ya Twende sawa zitachukua takribani miezi miwili na zitakuwa na matukio mengi ...

Like
292
0
Monday, 16 March 2015
WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA JAMII YA UWEKEZAJI
Local News

WANANCHI wametakiwa kujitokeza na kujiunga na mifuko ya jamii ya uwekezaji  wa pamoja ya UTT AMIS ili kunufaika na faida mbalimbali za uwekezaji zinazotokana na kuongezeka kwa thamani ya vipande kufuatia kukua kwa mifuko hiyo ya uwekezaji kwa asilimia  25 kutoka bilioni 179 na kufikia bilioni 227 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita . Akisoma ripoti ya mifuko hiyo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Afisa mwendeshaji mkuu wa UTT AMIS Simon  Migangala amesema hayo ni...

Like
245
0
Monday, 16 March 2015
TAASISI ZA UKUSANYAJI FEDHA NCHINI ZIMETAKIWA ZIMETAKIWA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE KUWEZESHA BAJETI
Local News

WAKATI Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza Machi 17 mwaka,Taasisi za ukusanyaji fedha nchini  zikiwemo Halmashauri zimetakiwa  kutekeleza wajibu wake, ili kuwezesha lengo la Bajeti kufikiwa badala ya kutegemea fedha kutoka Hazina pekee. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU  NCHEMBA wakati akizungumza na EFM kuhusu changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Bajeti, ambapo amesema Halmashauri zikiwajibika ipasavyo kukusanya fedha na Wizara zenye wajibu wa kukusanya Maduhuli zikitekeleza kazi...

Like
252
0
Monday, 16 March 2015
POLISI DODOMA YASHIKILIA WAHAMIAJI HARAM 64 RAIA WA ETHIOPIA
Local News

POLISI Mkoani Dodoma wanawashikilia Wahamiaji Haram 64 Raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akiwa amefariki. Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia Dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea Kusini mwa Afrika. Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira...

Like
413
0
Monday, 16 March 2015
WIZARA YA MAJI NA JESHI LA POLISI LAFANYA KAMPENI KUSAKA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI KINONDONI
Local News

WIZARA ya maji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni imefanya Operesheni ya kukamata wezi wanaoiba  Miundo mbinu ya maji ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali jijini dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  PAUL MAKONDA amesema kuwa, katika oparesheni hiyoWilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya ya Mkoa wa Dar es salaam zilizohujumiwa na kuwa na wizi mkubwa wa maji katika miundo...

Like
267
0
Friday, 13 March 2015
BASI LA ARUSHA EXPRESS LAPATA AJALI LEO
Local News

BASI la Arusha Express limepata ajali leo maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kisongo jijini Arusha wakati likijaribu kulipita gari ligine na kukutana na lori mbele yake. Imeelezwa kuwa ili kuepusha madhara, dereva wa lori aliamua kuingia kichakani ili asigongane uso kwa uso na basi hilo. Katika ajali hiyo, hakuna aliyepoteza maisha isipokuwa watu ndani ya lori ndiyo wamejeruhiwa na kukimbizwa...

Like
718
0
Friday, 13 March 2015
PAC YAMTIMUA NAIBU GAVANA WA BOT NA BAADHI YA MAOFISA WAANDAMIZI
Local News

NAIBU Gavana wa Bank Kuu-BOT, JUMA RELI na baadhi ya maofisa Waandamizi wa Bank hiyo wametimuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali-PAC. Hatua hiyo ya kufukuzwa imekuja baada ya kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu uwepo wa Watanzania ambao wanatajwa kuwa wamefungua Akaunti nje ya nchi wakati sheria inakataza. Akizungumzia uamuzi huo jijini Dar es salaamMwenyekiti wa PAC Mheshimiwa KABWE ZITTO amesema kimsingi BOT wanaonekana kutojiandaa kuhusiana na Sakata hilo hivyo ni vema waende kujipanga...

Like
350
0
Friday, 13 March 2015
SAKATA LA KUSHAMBULIWA KWA ALIEKUWA MLINZI WA DK SLAA LACHUKUA SURA MPYA
Local News

SAKATA la kushambuliwa kwa aliyekuwa Mlinzi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dokta WILBROAD SLAA ,KHALID KAGENZI ,limechukua sura mpya baada ya kiongozi huyo kufika Katika kituo Kikuu Cha Polisi na kuandika maelezo takribani saa Tano. Hivi karibuni Dokta SLAA kupitia kwa mmoja wa Viongozi wa CHADEMA,MABERE MARANDO, alidai kuwepo kwa mpango wa kumdhuru ambao unaratibiwa na Maofisa wa Usalama kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa CCM. Mpango huo ulidaiwa kuwa ungetekelezwa kupitia kwa KAGENZI, ambaye baadaye aliteswa na kushambuliwa na...

Like
310
0
Friday, 13 March 2015
AFRIKA MASHARIKI HUENDA ISINUFAIKE NA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA DUNIANI KWAKUKOSA VIFAA VYA KUHIFADHIA MAFUTA
Local News

UTAFITI uliofanywa na kampuni ya Deloite East Africa umeonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa nchi za Afrika ya Mashariki kutofaidika na kushuka kwa bei ya mafuta duniani kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta hayo. Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Kodi wa kampuni hiyo JOSPEH THOGO ambapo amesema kuwa Kushindwa kwa nchi hizo za Afrika Mashariki kuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta kunamaanisha kuwa nchi hizo zitashindwa kujikusanyia mafuta ya kutosha kwa bei nafuu...

Like
402
0
Thursday, 12 March 2015
WIZARA YA FEDHA YATILIANA SAINI MIKATABA NA BENKI YA DUNIA
Local News

WIZARA ya fedha imetiliana saini mikataba mitatu na benki ya dunia itakayowezesha kuipatia serikali ya Tanzania mikopo ya miradi mitatu ya kuendeleza jiji la Dar es salaam, mradi wa kuendeleza ujenzi wa nyumba za bei nafuu na mradi wa uvuvi wa kikanda wa kuendeleza uvuvi, yenye ujumla ya thamani ya dola milioni 396 sawa na shilingi bilioni 710. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dokta Servacius Likwelile ameahidi kuwa serikali...

Like
255
0
Thursday, 12 March 2015
WAPIGA RAMLI 225 MBARONI KUFUATIA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI
Local News

JUHUDI za kukomesha matukio ya kihalifu ya kuwaua watu wenye Ulemavu wa Ngozi Albino, zimeanza kuzaa matunda baada ya Jeshi la Polisi kuwashikilia wapiga ramli 225. Kushikiliwa kwa wapiga ramili hao kunatokana na Operation inayoendeshwa na Polisi ya kupambana na vitendo vya Kikatili ili kuhakikisha matukio hayo hayaendelei kutokea. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi ADVERA BULIMBA imeeleza kuwa wapiga ramli hao wamekamatwa kwenye Mikoa ya Tabora,Geita,Mwanza,Simiyu,Shinyanga,Kagera,Katavi na...

Like
244
0
Thursday, 12 March 2015