WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa WILLIUM LUKUVI ameaagiza maofisa Ardhi kuhakikisha wanatenda haki ya kutoa hukumu kwa wakati kuhusu mashauri ya ardhi. Mheshimiwa LUKUVI ameeleza hayo Katika ziara yake ya Siku mbili mkoani Mwanza na kuongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa. Pia amewaasa maofisa Ardhi kuhudumia wananchi kwa Haki na Uzalendo bila kujali uwezo wao...
KUMETOKEA ajali mbaya mjini Mafinga eneo la Changalawe Mkoani Iringa baada ya abiria wanaodhaniwa kufikiwa 40 , wa basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kuelekea Dar es salaam kufunikwa na kontena Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mongi ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo. Inasemekana idadi kubwa ya abiria hao wamefariki lakini Kamanda Mongi ameiambia EFM kwa njia ya simu kuwa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo itatolewa mara baada ya kukamilisha Zoezi la kuitoa miili...
KATIKA kudumisha Amani na Upendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais pamoja na Upigaji Kura za Maoni kwa Katiba mpya, Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha New Hope Family kimezindua Kikombe cha Amani na Upendo. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kituo hicho OMARI KOMBE amesema, Kikombe hicho kitazunguka maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhamasisha Watanzania kudumisha amani kama ilivyodumishwa na aliyekuwa Baba wa Taifa Mwalim JULIUS NYERERE Pia KOMBE amelaani Vitendo vinavyofanywa na...
WATANZANIA wametakiwa kupambana na ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi ili kupunguza mazalia ya Mbu wanaosababisha ugonjwa huo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Dokta MWELE MALECELA wakati akitoa taarifa ya Utafiti wa Mlipuko wa Dengue jijini Dar es es salaa uliofanywa na Taasisi yake. Dokta MALECELA amesema lengo la Utafiti huo ni kukusanya takwimu za kiwango cha maambukizi ya Dengue kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya kutolea...
KITUO Cha Radio Cha EFM kimezindua rasmi Kampeni yake ya TWENDE SAWA ikiwa ni kuashiria Shamrashamra za kutimiza Mwaka MMoja tangu kuanzishwa kwake. Akizungumzia shamrashamra hizo Mkuu wa Vipindi wa Efm DICSON PONELA amesema sherehe hizo zimeshaanza rasmi kwa matukio mbalimbali ambapo tarehe rasmi ya sherehe hizo ni April Pili mwaka...
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Figo-NESOT pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya na Magonjwa ya Figo, imeeleza kuwa Ugonjwa wa Figo wa Mstuko na Ugonjwa Sugu wa Figo ni tatizo mojawapo kwenye kundi la magonjwa yasiyoambukiza ambayo mchango wake katika kuongeza athari za Kiafya na Vifo Ulimwenguni unaongezeka siku hadi siku. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo, Dokta JACKLINE SHOO amesema Tanzania ni nchi...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Leo kimemvua Rasmi Uanachama aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa ZITTO KABWE kwa madai ya kushindwa kutekeleza Masharti ya Katiba ya chama hicho. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Mheshimiwa TUNDU LISU amesema kuwa, mnamo mwaka jana Mheshimiwa ZITTO alifungua Mashitaka katika Mahakama Kuu akizuia vyombo vya Chama kukaa kujadili na kufanya maamuzi yanayohusu yeye kuendelea kuwa Mwanachama wa Chama hicho. Amesema kuwa katika kipindi...
HALMASHAURI ya WIlaya ya Babati Mkoani Manyara,imekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 39 kwa kikundi cha Kuweka na Kukopa cha Vijana SACCOSS na vikundi vitano vya Wanawake 150. Akikabidhi hundi hizo Katika Kijiji cha Ayasanda,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo NICODEMUS TARIMO,amesema fedha hizo zinatokana na Asilimia 10 ya Mapato ya Halmashauri kwa ajili kuwawezesha Vijana na...
CHAMA cha Mapinduzi-CCM kimeonyesha kuridhishwa na harakati za Mwenyekiti wake Rais JAKAYA KIKWETE,Katika kutekeleza Ilani yao juu ya ushirikishwaji wa Wanawake katika Uamuzi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, ABDULRAHMAN KINANA katika Ziara yake ya kuangalia Utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita katika Kijiji cha Mageleko. KINANA amesema amezunguka sehemu kubwa ya mkoa huo na kukuta nafasi nyingi za juu zikishiliwa na Wanawake hali inayoonyesha kuwa Utekelezwaji wa Ilani ya CCM umeafanikiwa kwa kiasi...
WANAWAKE nchini wamehimizwa kuachana na malumbano na badala yake wameshauriwa kuondoa hofu na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani na nje ya chama katika ngazi za mikoa na Taifa lakini pia wajitokeze kuomba nafasi ambazo zitawaniwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu . Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi-ACT, MOHAMED MASSAGA kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8....
UBALOZI wa Uingereza nchini leo umekutana na wadau mbalimbali ikiwemo Jeshi polisi na Mahakama kwa lengo la kutoa mafunzo yatakayowasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku kwa manufaa ya Taifa. Akizungumza wakati wa utoaji mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam mshauri mkuu wa masuala ya kimahakama kutoka Ubalozi huo LINDSEY MCNALLY amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia kutatua kwa haraka kesi nyingi za kimahakama zinazochukua muda mrefu....